Bwana Abdiweli Sheikh Ahmed ateuliwa kuwa Waziri mkuu mpya wa Somalia
Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia amemteua na kumtangaza Bwana Abdiweli Sheikh
Ahmed kuwa Waziri mkuu mpya wa Somalia. Itakumbukwa kwamba, tarehe 2 Desemba 2013,
Bunge la Somalia lilipiga kura ya kutokuwa na imani na aliyekuwa Waziri mkuu wa Somali
Bwana Abdifarah Shirdon, aliyeondolewa madarakani kwa kura 250 dhidi ya kura 184 zilizotaka
aendelee kubaki madarakani.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema, kura
hii ya maoni inaweza kupelekea kuanguka kwa Serikali iliyoko madarakani. Baada ya
Bunge kuridhia uteuzi wa Bwana Abdiweli Sheikh Ahmed ambaye kitaaluma ni mwanauchumi
kuwa Waziri mkuu, atakuwa na siku 30 za kupanga tena upya Baraza la Mawaziri nchini
Somalia.