2013-12-13 10:33:13

Afrika ya Kusini inamlilia Tata Madiba!


Maelfu ya waombolezaji yamejipanga mistari ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Nelson Mandela, ambaye mwili wake umewekwa kwenye Ofisi za Serikali, mjini Pretoria, Afrika ya Kusini, kabla ya mazishi yake, yatakayofanyika Kijijini kwake Qunu, kilichopo katika Jimbo la Cape Mashariki, Jumapili tarehe 15 Desemba 2013.

Serikali ya Afrika ya Kusini inasema haina uhakika kwamba, maelfu ya watu waliojipanga kwa nia ya kutaka kutoa heshima zao za mwisho kwa Tata Madiba wataweza kufanikiwa kabla ya muda uliowekwa, ili kuuandaa mwili wa Mzee Nelson Mandela kwa maziko, jumapili ijayo.







All the contents on this site are copyrighted ©.