2013-12-11 15:22:14

Vatican, Ijumaa kuwasha rasmi, taa za mti wake wa Krismas


Taarifa imetolewa kwamba, taa za Mti wa Krismasi uliowekwa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambao ulitolewa huko Waldmünchenu Ujeruman, taa zilizopamba mti huo, zitawashwa rasmi Ijumaa,13 Desemba, majira ya saa kumi na nusu za jioni.

Taarifa hiyo , kutoka Ubalozi wa Ujerumani katika Jimbo Takatifu, inasema, hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1984, kwa mti wa Krismasi unaowekwa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutoka Ujerumani, kutoka mji wa Waldmünchenu wa Upper Palatinate Ujerumani.

Kwa ajili ya tukio la kuwasha taa zilizopamba mti huo, utakuwepo ujumbe mkubwa wa uwakilishi wa mkoa wa Waldmünchenu, ukiongozwa na Askofu Rudolf Voderholzer wa Regensburg, akiwepo pia Rais wa kile kinachoitwa Frenckfestspiele, bwana Franz Löffler na pia ujumbe kutoka Jamhuri ya Czech, Askofu František Radkovský wa jimbo la Pilsen. Aidha serikali ya Bavaria itawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ulaya na Mahusiano ya Mkoa , Dk Beate Merk . Na Serikali ya Shirikisho la Ujeruman, itawakilishwa na Katibu wa Wizara ya Shirikisho kwa ajili ya ulinzi utamaduni wa Mkristo, Mheshimiwa Schmidt.








All the contents on this site are copyrighted ©.