Papa Francis anakutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo, Denis Sassou N'guesso
Jumatatu 09.12. 2013, Papa Francisko alikutana na Rais wa Jamhuri ya Congo , Mheshimiwa
Denis Sassou N'guesso . Taarifa iliyotolewa na Vatican inasema, Baba Mtakatifu
Francisko na mgeni wake , walizungumzia zaidi mchango wa Kanisa Katoliki kwa watu
wa Congo, hasa katika nyanja ya afya na elimu. Na pia waligusia uhusiano kati ya
Jimbo Takatifu na Jamhuri ya Congo na kuahidi kuimarisha ushirikiano baina ya nchi
hizi mbili. Na mwisho, walibadilishana mawazo juu ya hali ya kisiasa katika Jamhuri
ya Afrika ya Kati ambapo waasi Kiislamu wa Seleka, wanaendesha kampeni ya ugaidi dhidi
ya raia na dhidi ya makanisa ya Kikristo. Walikubaliana kwamba kuna haja ya kuwa
makini hasa katika utoaji wa huduma kwa wakimbizi na watu walio timuliwa makwao ,
na kushughulikia kwa kina zaidi , tatizo la ukosefu wa usalama katika kanda hiyo
ikiwa ni pamoja na kukua kwa wimbi la ubabe wa kupindukia.