2013-12-10 15:28:50

Jimbo la Papa lasema, mkutano wa Bali ni fursa mpya kusimamia ukuaji wa biashara huria yenye usawa zaidi .


Askofu Mkuu Silvano Tomas, Mtazamaji wa kudumu wa Jimbo la Papa katika ofisi za Umoja wa Mataifa za Mjini Geneva, wiki iliyopita tarehe 4 Desemba, alishiriki katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa Mawaziri wa Biashara na Shirika la Biashara duniani "WTO". Mkutano uliofanyika mjini Bali Indonesia .
Akichangia maoni katika mkutano huo, Askofu Mkuu Silvano, alitoa angalisho zaidi katika sababu zinazoleta mkwamo katika uchumi wa dunia, huku akionyesha kujali kwamba, licha ya uwepo wa shughuli nyingi za kiuchumi katika nchi nyingi zilizoendelea na mipango mingi ya uchumi,bado soko la dunia linachechemea, kwa kuteswa na madhara ya sera mbovu za uchumi na fedha duniani, ikiwemo kukosekana kwa taratibu za endelevu katika mifumo ya fedha , kukosekana kwa usawa ndani ya nchi na kimataifa.

Aidha alitaja jinsi uzoefu na tafiti katika uchumi, zinavyo onyesha kwamba, mgogoro wa fedha, ndiyo chimbuko la hali ngumu za maisha ambao si tu umeathiri karatasi ya mzania wa urari katika taasisi za fedha, lakini pia kishindo chake kusikika pia serikalini na sekta binafsi. Vizuizi na masharti magumu yanayowekwa katika sera za fedha, inakuwa ni vikazo katika kukabiliana ulipaji wa madeni,ambako tayari kuna chochewa na hali nyingine mbalimbali zinazo hatarisha uchumi katika nchi mbalimbali.
Aidha aliitoa angalisho kwamba, wakati wachache wanaonja hali ya kuibuka kutoka umaskini, pia kuna kukua kwa pengo kati ya wanaoibuka katika mafanikio na wale walio bado katika shimo la Umaskini wa kukithiri. Ametaja haya ni matokeo ya ukosefu wa usawa, unaoshamirishwa na itikadi mbovu katika kulinda uhuru kamili ya soko na matarajio ya fedha, yanayo kuzwa na moyo wa tamaaa na utafutaji wa faida binafsi bila kujali kuumiza wengi .
Jimbo la Papa limesema, kama kweli dunia inataka sauti uchumi wa dunia isikike katika hali ya usawa, kinachohitajika zaidi kwa wakati huu, ni uwepo wa njia bora zaidi katika mwingiliano wa utendaji wenye kuheshimu uhuru wa kila taifa ,na kuhakikisha ustawi wa uchumi kwa nchi zote na si nchi chache tu .

Na kwamba, Mkutano wa Bali, unao uwezo wa kupiga hatua muhimu kuelekea kuundwa kwa kitu kipya ndani ya Shirika la Biashara Duniani, jambo linalo weza kutoa fursa nyingine , katika ubunifu wa mfumo wa mazungumzo ya kimataifa. Mkataba wenye uwiano na haki kwa ajili ya uwezeshaji wa kibiashara ndani ya uwezo wa dunia. Kwa hiyo inawezekana kufikia hilo kupitia mkutano huo wa Bali. Uwepo wa fursa mpya ya kusimamia, zaidi ya yote, ukuzaji wa biashara huria na usawa zaidi , si kama mwisho wa yote, lakini kama moja ya zana nyingi za kukomesha umaskini kwa wote.









All the contents on this site are copyrighted ©.