2013-12-09 15:47:37

Papa asema , sasa basi kwa uadui na migawanyiko Misri na Mashariki ya Kati.


Baba Mtakatifu Francisko amerudia kutoa ombi la kufikishwa mwisho wa migwanyiko na uadui nchini Misri na Mashariki ya Kati kwa ujumla. Ni wito wa Papa wa mapema Jumatatu hii, wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican. Papa aliongoza Ibada hii, akishirikiana na Mkuu wa Kanisa Katoliki la Kikoputiki, Upatriaki wa Alexandria, Patriaki Ibrahim Isaka Sidrak. Uwepo wao katika Ibada hii ya pmoja unatajwa kuwa kielelezo dhahiri cha usharika na umoja na Khalifa wa Mtume Petro.
Katika homilia yake, Papa Francisko, alitaja jinsi anavyoguswa na maisha ya Wakristo nchini Misri, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipita katika vipindi vigumu vya ukosefu wa usalama na vurugu. Kwa muono huo, alirudia kutaja mshikamano wake na Wakristu hao, na kurudia kutoa upya ombi lake, kwa ajili ya uhuru wa dini nchini Misri na Mashariki ya Kati kwa ujumla.

Papa alieleza kwa kurejea uaminifu wa Wakristu hao katika imani yao kwa Kristu akitazamisha katika maneno ya Nabii Isaya katika somo la kwanza, ambamo mnatolewa onyo kwa mioyo kuwa macho, katika kipindi cha kusubiri kwa ujio wa Bwana. Alieleza kwa kutazama jinsi mioyo ya wafia dini, inavyoutia ujasiri mioyo ya Wakristu wa Misri, wanaoendelea kupambana na ukosefu wa amani na ghasia , bila kukata tamaa, kwa sababu ya imani yao, imeoteshwa juu ya imani imara kwa Kristo. Aliwahiza na kuwatia shime, waendelee kuwa na ujasiri huo, na kamwe wasiogope.

Na alimshukuru Mungu kwa kumwezesha kukutana na Kiongozi wa Kanisa Misri, Patriaki Sidrak, na hivyo kumwezesha kumthibitishia mshikamano wake na udugu na Waamini Wakatoliki Wakoputiki wa Misri, akisema, kukutana kwao kumeweza kuwaimarisha zaidi katika tumaini lao moja.

Papa akitoa tafakari juu ya somo la Injili, tunapata fundisho msingi kwamba, mbele ya Kristu , udhaifu wa mwili wa mwili wa binadamu si kitu.Kristu anao uwezo wa kuushinda uovu wote wa binadamu na ulemavu wa dhamiri unaozidi kuenea. Kwa makosa ya umaskini wa kiroho na historia ya dhambi zetu – aliongeza, dhambi huweza kujipenyeza katika miundo ya kijamii na kuwa kutia giza katika uelewa wa kiroho, juu ya mambo haya. Lakini, tunafarijika kwamba,Kristu anaweza kubadili udhaifu huo mara moja, kwa kuwa Yeye ana mamlaka juu ya mamlaka yote. Amri Yake, inaweza kubadili hali yote, kusema "ondoka na tembea".

Kwa tumaini hili, Papa alitoa wito kwa waamini kutolea maombi yao, kuiombea nchi Tya Misri , Nchi Takatifu, na Mashariki ya kati, ili iwe na ujasiri wa kujiamini, na kujinasua katika makucha ya uadui na mgawanyiko.
Papa aliomba, Mwanga wa Kristu uweze kuangazia mikataba ya amani, inayotiwa giza na uvuli wa maslahi na mamlaka, na hatimaye ipatikane dhamana halisi ya uhuru wa dini kwa watu wote, ikiwemo haki ya Wakristo wa eneo hilo, kuishi kwa amani katika nchi yao ya kuzaliwa, na taifa pendwa la Misri lililoshirikishwa katika historia ya binadamu kukombolewa.

Papa alieleza kwa kukumbuka kwamba, Familia Takatifu ya Nazareth, ilikimbilia katika taifa hili la Misri .

Na Patriaki Sidrak,akitoa hotuba wakati wa ibada hiyo, aliionyesha furaha yake ya kukutana na Papa, na jinsi Papa alivyoonyesha ukaribu wake na watu wa Misri, naUpatriaki wote wa Alesandria, ambako anasema, kwa wakati huu wanahitaji sana msaada Baba, Mrithi wa Kiti cha Mtume Petro.
Pamoja , sasa shukrani za kina kwa Papa kutoka kwa Maaskofu, Mapadre , watawa wake kwa waume na waamini wote wa Coptic Kanisa Katoliki , na pia Kardinali Leonardo Sandri , Mkuu wa Usharika kwa Makanisa ya Mashariki, Patriaki Ibrahim Isaak Sidrak ,alitaja kwamba, kipindi hiki wanachopita, kwao ni wakati nyeti wa kihistoria, ambamo wanahitaji kuungwa mkono na kukumbatiwa na Utakatifu wa kiti cha Petro kwa ajili ya kanisa lake Kristu, hasa katika maadhimisho ya kipindi hiki cha sherehe za Umwilisho wa Neno.
Na alimshukuru Papa kwa waraka wake wa "Furaha ya Injili “(Evangelii gaudium), iwe mwanga wa Siku Kuu ya Noel, nyota ya asubuhi inayo onyesha njia ya upendo, umoja , maridhiano na amani , zawadi ambayo Dunia ya Misri inaihitaji sana. Na alitoa mwaliko kwa Papa Francisko kuitembelea Misri.








All the contents on this site are copyrighted ©.