2013-12-09 09:20:39

Maria Mkingiwa dhambi ya Asili ni tunda la Upendo wa Mungu- Papa




Maria kutungwa mimba bila dhambi ya asili, ilivyo andikwa katika mpango wa Mungu, ni tunda la upendo wa Mungu, kuikomboa dunia dhidi ya dhambi, Baba Mtakatifu Francisiko alieleza wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , siku ya Jumapili, mbele ya mahujaji na wageni waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Hotuba fupi ya Papa ililenga katika Siku Kuu ya Maria Mkingwa dhambi ya Asili, ambayo pia ilikuwa ni Jumapili ya Pili ya Kipindi cha Majilio.

Papa aliendelea kuitafakari sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, akisema, katika Siku kuu hii, macho yetu tunayaelekeza katika uzuri wa Mama wa Yesu , Mama Yetu, na kwa furaha kubwa , Kanisa linatafakari maneno ya Mtakatifu Luka “ amejaa neema" kama ilivyoandikwa katika Injili ya Luka ( Lk 1:28). Bikira Maria Mama yetu, zaidi ya yote, anatuongoza sisi katika mwendo wetu tunapoelekea kuisherehekea Siku Kuu ya kuzaliwa mwanae Yesu Kristu, Siku Kuu ya Noel. Maria Mkingiwa dhambi ya asilia, anatufundisha jinsi ya kuishi wakati huu wa kusubiri ujio wa Bwana.

Papa alifafanua zaidi kwamba, Maria kukingiwa dhambi ya asili tangu wakati wa kutungwa mimba , iliandikwa katika mpango wa Mungu, na ni tunda la upendo wa Mungu, katika kumkomboa binadamu dhidi ya dhambi.

Baada ya kuongoza sala ya Malaika wa Bwana , Papa alionyesha ukaribu wake kwa Kanisa Amerika Kaskazini,ambako lilikuwa likisherehekea miaka 350 ya Parokia yake ya kwanza ya Mama Yetu wa Quebec “Notre- Dame de Québec”.Na ahitimisha kwa kuwatakia wote, Siku Kuu njema ya Mama Yetu Mkingiwa dhambi ya Asili.








All the contents on this site are copyrighted ©.