2013-12-09 08:47:02

Jubilee ya miaka 50 ya Uhuru wa Kenya!


Serikali ya Kenya imetangaza kwamba, tarehe 13 Desemba 2013 itakuwa ni siku ya mapumziko kitaifa, ili kuwapatia wananchi wa Kenya fursa ya kusherehekea Jubilee ya Miaka 50 tangu Kenya ilipojipatia uhuru wa bendera kutoka kwa Mwingereza. Taarifa zinaonesha kwamba, maandalizi ya Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya yamekamilika.

Wananchi wa Kenya wanaendelea kuhamasishwa ili kuhakikisha kwamba, Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya, inakuwa ni fursa nyingine tena ya kujizatiti katika kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa; kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa kuongeza: bidii, juhudi na maarifa katika shughuli za uzalishaji na utoaji huduma.

Kilele cha Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya, ni Usiku wa manane hapo tarehe 12 Desemba 2013, Bendera ya Taifa itakapopandishwa kwa mara nyingine tena, kama ilivyofanyika mwaka 1963.








All the contents on this site are copyrighted ©.