Mheshimiwa Padre Georges Bizimana ateuliwa kuwa Askofu mwandamizi wa Jimbo Katoliki
Bubanza, Burundi
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Georges Bizimana kuwa Askofu mwandamizi
wa Jimbo Katoliki la Bubanza, nchini Burundi. Askofu mwandamizi Bizimana ambaye kwa
asili anatoka Jimbo Katoliki la Ngozi, hadi uteuzi wake, alikuwa ni Gombera wa Seminari
kuu ya Jean Paul II, iliyoko Jimbo Katoliki la Gitega, Burundi.
Alizaliwa
tarehe 12 Machi 1965, huko Buraniro, Jimbo Katoliki la Ngozi. Baada ya masomo na majiundo
yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 20 Agosti 1994. Baadaye akaendelea na masomo
ya juu kuhusu taalimungu maadili mjini Roma. Tangu alipopadrishwa amewahi kuwa mlezi
Seminarini, Paroko msaidizi Parokia ya Gasenyi, Paroko wa Parokia ya Mubuga na mkurugenzi
wa miito.
Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2008 alikuwa mjini Roma kwa ajili
ya masomo, kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Alfonsiani. Mwaka 2008 hadi mwaka 2010
alikuwa ni Jalimu na kuanzia Mwaka 2010 hadi uteuzi wake alikuwa ni Gombera wa Seminari
kuu ya Jena Paul II.