2013-12-06 14:20:08

Rais Mstaafu Nelson Mandela ameaga dunia


Afrika Kusini na dunia kwa ujumla iko katika maombolezo ya kuondokewa na mtu mashuhuri duniani,Nelson Madiba Mandela, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, na mshindi wa Tuzo ya Amani, ambaye amefariki dunia kwa homa ya mapafu. Nelson Madiba Mandela alifariki usiku wa Alhamis kuamkia Ijumaa, akiwa na umri wa miaka 95 na alikuwa na umri wa miaka 95.

Nelson Madiba Mandela, dunia inamkumbuka kama mfano wa mtu wa amani, msahemevu na shujaa, aliye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wachache wabaguzi wa rangi, baada ya kufungwa jela kwa miaka 27. Pia anaheshimiwa kuwa nembo ya kiongozi adilifu duniani.

Rais Jacob Zuma, alitangaza habari za kifo cha Mandela Alhamisi usiku kwenye televisheni, akisema Nelson Mandela aliyejulikana kwa jina la ukoo , Madiba, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, majira ya 20:50, Desemba 05, 2013 akiwa nyumbani kwake, karibu na familia yake.

Rais Zuma amesema, Yeye sasa kapumzika. Yeye sasa yuko katika amani ya kudumu. Afrika Kusini imepoteza mwana wake mkuu, na Baba wa taifa. '
Mara baada ya habari za kifo cha Nelson Mandela, kutangazwa , nchini Afrika Kusini , wakazi wa kitongoji cha Soweto, ambako kuna weusi wengi, walikusanyika katika mtaa wa karibu na nyumba ambapo yeye Nelson Mandela aliwahi kuishi. Waliimba na kucheza kwa kuomboleza kifo chake, kama ilivyo mila na desturi za utamaduni wao.

Kwa heshima yake , bendera zote za kitaifa, zinapeperuka nusu mlingoti mpaka baada ya mazishi, ambayo tarehe bado kutajwa. . Na habari tokea mtaa wa Houghton kitongoji cha Johannesburg ambako kuna nyumba yake, watu walikusanyika, wakiwa na simanzi za kusisimua , ambako baadhi waliimba nyimbo za maombelezo , na wengine walipiga mbiu ya vuvuzela, na picha zenye sura ya Mandela akitabasamu zilizotundikwa juu ya miti kukiwa na maneno Madiba pumzika kwa amani, Pia watu wametengeneza kaburi la bandia ambako wameweka mishumaa , bendera za taifa na mashada ya maua.


Historia ya Nelson Madiba Mandela :
1918 Alizaliwa katika mkoa wa Eastern Cape , katika familia , kitemi. Mandela alikulia kijijini, ambako alipata mafunzo mazuri ya kuwa kiongozi, na baba yake alifariki na kumuacha katika umri wa miaka tisa. Mandela katika maisha yake alisifu malezi aliyoyapata kutoka kwa baba yake ambaye alipenda utu wema na uadilifu katika maisha.
Nelson Mandela alikuwa muumini wa kanisa la Methodist, alisoma katika shule ya Kimethodist na alipita katika vyuo vikuu mbalimbali , Chuo Kikuu cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Afrika Kusinina Chuo Kikuu cha Witwatersrand.

Mwaka 1943 akajiunga na chama cha ANC . Na kwamba ndoa zake mbili za kwanza zilivunjika kutokana na yeye kuchukua muda mwingi zaidi katika masuala ya kisiasa.

Alifunga ndoa na Mke wake wa Kwanza Evelyn Wase, 1944 na walizaa watoto watatu na waliishi maisha mazuri. Lakini mwaka 1954 wakati Mandela alipokamatwa kwa makosa ya uhaini kwa mara ya kwanza , na kuwekwa jela na baadaye kutolewa baada ya kuwekewa dhamana , Mandela alimkuta mkewe kaondoka na kuacha watoto wao wadogo wawili. Everlyn alirudi kwao na baadaye kuolewa na mwanaume mwingine.

Baadaye, katika harakati za kisiasa, Mandela alikutana na Winnie Madikizela , wakati alipokamatwa mara ya pili kwa kesi ya uhaini na kufungwa kwa miaka miwili. Kunako mwaka 1958 walifunga ndoa na Winnie Madikizela na walizaa watoto wawili wa kike, kabla Mandela hajafungwa gerezani mwaka 1964. Na baada ya kuhukumiwa kifongo cha maisha,maisha yao kama mke na mme yaliendelea kwa njia ya barua na Winnie kumtembelea gerezani,hadi Mandela alipoachiwa huru mwaka 1990, Winnie alimchukua Mandela kama mme , lakini kumbe wakati huohuo, kifichoni alikuwa na bwana mwingine kijana zaidi. Na mwaka 1992, walitangaza kutengana rasmi.

Na mke wa tatu, Graca Machel, alianza kufahamiana na Nelson Mandela mwaka 1986 baada ya kifo cha mmewe Samora Michel. Mwaka 1996 , Nelson na Graca walifungishwa ndoa na Rais Robert Mugabe, ambaye ameishi nae muda wote hadi kifo chake, lakini hakuzaa nae mtoto.

Watoto wa Nelson Madiba Mandela ni Madiba Thembekile Mandela. Makaziwe Mandela, , . Zenani Mandela, Zindziswa Mandela.

Maisha ya kisiasa kwa ufupi yanataja :
Alijiunga na ANC mwaka 1943.
1956 Alifunguliwa kesi ya uhaini lakini baada ya miaka minne kiasi ikafutwa.
1962 Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano.
1964 Alishitakiwa kwa kosa la kuhujumu serikali na kupewa hukumu ya kifungo cha maisha.
1990 Aliachiliwa huru kutoka gerezani, na
1993 alitajwa kuwa mshindi wa tuzo heshima ya Amani.
1994 alichaguliwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini.
1999, aliachia madaraka hayo.
2001 Aligunduliwa kua na Saratani ya tezi kibofu
2004 alitangaza kustaafu maisha ya kisiasa.
2013 Desemba 5, amefariki dunia








All the contents on this site are copyrighted ©.