2013-12-06 12:18:26

Msichoke kusali!


Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha, kilichoko mjini Vatican siku ya Ijumaa, tarehe 6 Desemba 2013 amewataka waamini kujenga moyo na bidii ya sala bila kuchoka wala kukata tamaa kama walivyofanya wale wakoma wanaosimuliwa kwenye Injili, yule Mama mjane na Kipofu aliyepaza sauti yake hata Yesu akaweza kumsikiliza na kumponya! Waamini waendelee kubisha hodi, iko siku Yesu atawasikiliza na kuwatekelezea haja zao kadiri ya upendo wake.

Waamini wanaposali wawe na imani thabiti na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ni mweza wa yote, wakimwomba anaweza kuwatekelezea. Kama binadamu wanaelemewa pia na dhambi ambayo ni kikwazo katika ujenzi wa uhusiano mwema na Mwenyezi Mungu; wawe na ujasiri wa kusema ukweli, ili watubu na kumwongokea Mungu.








All the contents on this site are copyrighted ©.