2013-12-05 09:14:19

Vatican inaendelea kujizatiti katika mapambano dhidi ya utakatishaji wa fedha haramu inayoweza kugharimia vitendo vya kigaidi!


Mamlaka ya Habari za Kifedha mjini Vatican, AIF, tarehe 4 Desemba, 2013 imetiliana sahihi itifaki ya makubaliano na Mamlaka ya Habari za Kifedha nchini Ujerumani, BKA, Itifaki hii imetiwa sahihi na Kardinali Attilio Nikora, Rais wa Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican na kwa upande wa Ujerumani, Bwana Michael Dewald, Mkurugenzi wa BKA ametia sahihi.

Lengo ni kuendelea kushirikiana katika ngazi ya kimataifa katika mapambano dhidi ya utakatishaji wa fedha haramu inayoweza kutumiwa katika kugharimia vitendo vya kigaidi sehemu mbali mbali za dunia.







All the contents on this site are copyrighted ©.