2013-12-04 09:19:41

Mti wa Noeli kuwasili kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro hapo tarehe 6 Desemba 2013


Kardinali Crescenzio Sepe, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Napoli ndiye aliyetoa zawadi la Pango la Noeli kwa Mwaka 2013 kwa Baba Mtakatifu Francisko. Mti wa Noeli utakaosimikwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro umetolewa na Jumuiya ya Waldmunchen kutoka Bavaria, Ujerumani.

Mti huu unatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro hapo tarehe 6 Desemba. Una urefu wa mita 25 na uzito wa tani 7.2. Shughuli za kupamba Pango la Noeli zitafanywa na wafanyakazi wa Vatican. Baada ya Sherehe ya Noeli, mti huo utapasuliwa mbao ambazo zitatumika kwa ajili yakutengenezea vifaa vya michezo kwa watoto na matumizi mengine ya kawaida!







All the contents on this site are copyrighted ©.