2013-12-04 10:49:37

Dr. Asha-Rose Migiro ateuliwa kuwa Mbunge!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dokta Asha-Rose Migiro, aluyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dokta. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza Desemba 2, 2013. Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.








All the contents on this site are copyrighted ©.