2013-12-03 10:21:48

Juhudi za kukoleza mchakato wa majadiliano ya Kiekumene na Kanisa la Kiorthodox nchini Romania


Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo pamoja na ujumbe wake, kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 7 Desemba 2013 wako nchini Romania kuangalia mwamko wa majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Wakristo na kuanza mchakato wa majadiliano na Kanisa la Kiorthodox nchini Romania.

Akiwa nchini humo, Kardinali Koch na ujumbe wake, watapata fursa ya kukutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa Makanisa ya Mashariki pamoja na kukutana na viongozi wa Baraka la Maaskofu Katoliki Romania. Ratiba inaonesha kwamba, Kardinali Koch amepangiwa pia kukutana na viongozi wakuu wa Serikali nchini Romania.







All the contents on this site are copyrighted ©.