Papa awaasa Wanafunzi: niniyi ni watendaji na si watazamani-
Papa amewahimiza wanafunzi wa vyuo vikuu kutoathiriwa na maoni ya kilimwengu yanayo
sababisha viwango vya maadili kummonyoko chini, lakini wadumishe moyo wa ujasiri
wa kubaki aminifu katika Maadili ya Kikristu na kanuni za kidini. Kwa kufanya wataweza
kupata nguvu na hekima za kusonga mbele na maisha adilifu, licha ya kupambana na mawimbi
ya kilimwengu. Ni kudhamiria kutembea kwa imani na kuishi sambamba na Injili, inayo
wasindikiza wakati wote huu wa kipindi cha majilio , na kuishi kwa uaminifu wa kiroho
Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana , Noel. Papa Francisko alitoa himizo hili Jumamosia,
alipokutana na walimu na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Roma ndani ya Kanisa la Mtakatifu
Petro, akiendeleza utamaduni wa siku nyingi wa Papa kuadhimisha Ibada ya Sala ya Masifu
kwa ajili ya kuzindua Jumapili ya kwanza ya majilio. Papa Francisko akihutubia,
alizungumzia Mungu kuingilia kati katika maisha ya muumini, kama ishara ya uaminifu
wake. Alieleza , Mungu anapenda kuingilia kati kwa sababu anafahamu asili ya binadamu
ni tete. Na Yeye ni aminifu kwa kazi yake aliyoianzisha kwa kila mmoja huumini ,
na daima huikamilisha. Na hili linampa muumini imani kubwa na uhakika wa usalama:
imani kwamba anakaa ndani ya Mungu lakini Mungu anahitaji ushirikiano wa waamini kukubali
kuongozwa nae na hasa katika utendaji wa maisha, na ushujaa wa kukabiliana na changamoto
za nyakati hizi. Papa aliendelea kuwaambia walimu na wanafunzi wa Vyuo Vikuu,
kwamba mapenzi yao na uwezo wao ukiunganishwa na Roho Mtakatifu aliyekuja kukaa kati
ya kila mmoja wao siku ya ubatizo , atawafanya kuwa watendaji na si watazamaji katika
changamoto cha nyakati hizi. Papa Francisko aliwatahadharisha wanafunzi kwamba,
wameitwa kukabiliana na changamoto nyingi na nzito, kwa kuwa na nguvu ya ndani na
ujasiri wa Injili. Na kwamba mazingira ya kijamii wanamoishi yanawalemea kutokana
na kuzidiwa na udhaifu na mchoko wa upweke. Papa amewatia moyo, akiwataka washinde
changamoto hizo kwa kuyakabidhi maisha yao katika upendo wa Injili , usiomtupa mtu,
na hivyo watasonga mbele na maisha ya kila siku bila kukata tamaa. Na amewataka wawe
na ujasiri wa kubuni miradi mikubwa mpya lakini isiyo nyakua shauku yao kama vijana.
Na itakuw ani makosa makubwa iwapo vijana watakubali kubaki wamefunga na fikra dhaifu
za kufanana.
Ni kudhamiria kutembea kwa imani na kuishi sambamba na Injili,
inayowasindikiza wakati wote huu wa majilio , na kuuiishi kwa uaminifu wa Roho wa
Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana , Noel. Mwisho wa Ibada hii, iliyohudhuriwa na
mamia ya wanafunzi waliojaza ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican,
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Brazil, walikabidhi Sanamu ya Bikira Maria, Kiti cha
Hekima na Mlinzi wa wanafunzi kwa ujumbe wa Ufaransa. Sanamu iliyochongwa na
msanii mashuhuri Padre Marko Ivan Rupnik. Sanamu hiyo ilikuwa imekamilisha hija
yake katikavyuo vikuu vya Brazil, ambako wanafunzi wamekuwa wakikusanyika na kutolea
sala zao na kwa sasainaaendelea na hija hiyo, nchini Ufaransa