2013-12-01 13:47:03

Mkutano wa dini mbalimbali waandaliwa Roma


Kwa ajili ya ujenzi wa umoja na mshikamano wa jamii nchini Italia, mjini Roma, tarehe 4 Desemba 2013, kutafanyika mkutano, utakao jumuiya wawakilishi wa dini mbalimbali, za wahamiaji na watu mahalia wa Italia, wasomi , wanautamaduni, vyama na jumuiya na taasisi mbalimbali za kijamii.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutnao kama huo kufanyika hapa Roma, na umeitishwa na Waziri wa ushirikiano wa kijamii nchini Italia , Waziri Ce'Cile Kyenge.
Lengo la mkutano ni wawakilishi kushirikishana maoni na fafanuzi juu ya ukweli wa tunu za dini. Ni wakati wa kupanua mawazo na ufahamu juu ya imani zingine , kwa ajii ya ujenzi wa amani, kuheshimiana na mshikamanowa jamii. Mratibu Mkuu wa mkutano huu ni Yohane Roger,
Mjumbe Maalum kutoka gazeti la Avvernire.

Kikao cha Tume ya Kimataifa Teologia
Tume ya Kimataifa ya Teolojia, inayoongozwa na Rais Askofu Gerhard Ludwig Müller,itakuwa na Kikao chake cha mwaka Vatican 2-6 Desemba 2013. Kazi za Kikao hicho , zitafanyika chini ya usimamizi wa Padre Serge Thomas Bonino , O.P. Katibu Mkuu.

Katika Kikao hiki , Tume itaendelea kutafakari mada kuu tatu muhimu; suala la imani kwa Mungu mmoja. Pili maana ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa katika muono mpana wa mafundisho ya kikristo. Tatu ni tatizo la Imani ya Kikristu kukubali. Mwishoni mwa kikao hiki, wajumbe wanatazamia kukutana na Baba Mtakatifu Francisko.








All the contents on this site are copyrighted ©.