2013-11-30 08:05:16

Ijue Liturujia ya Kanisa tayari kujimwaga kisawasawa kutangaza Injili ya Furaha


Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda kukushirikisha tafakari ya kina inayoletwa kwako na Askofu Salutaris Melchior Libena wa Jimbo Katoliki Ifakara ambaye pia ni Mwenyekiti Idara ya Liturujia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuhusu Liturujia na umuhimu wake katika maisha na utume wa Kanisa, wakati huu bado Kanisa linapoendelea kutafakari yaliyojiri kwenye Mwaka wa Imani sanjari na Jubilee ya Miaka 50 ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, tayari kutweka hadi kilindini ili kutangaza Injili ya Furaha kwa Watu wa Mataifa. RealAudioMP3

“‘Maana kwa njia ya liturujia, hasa Sadaka takatifu ya Ekaristi, “latimizwa tendo la ukombozi wetu’. Liturujia inasaidia kikamilifu waamini waonyeshe katika maisha yao na kuwadhihirishia wengine fumbo la Kristo na pia maumbile halisi ya kanisa la kweli. Kanisa kwa undani kabisa ni la kibinadamu na pia la kimungu, linaloonekana ndani yake, lenye bidii kubwa katika matendo na uradhi katika kutafakari, lililopo ulimwenguni lakini kama mwenye kuhiji. Hayo yote yamo ili yale ya kibinadamu ndani yake yaelekezwe kwa yale ya kimungu, yaonekanayo kwa yasiyoonekana, matendo kwenye kutafakari, yaliyopo yaelekee mji ujao tunakoelekea.

Hivyo Liturujia kila siku inawajenga wale waliomo katika Kanisa wawe hekalu takatifu la Bwana, makao ya Mungu katika Roho, mpaka kuufikia utumilifu wa Kristo. Wakati huohuo kwa namna ya ajabu Liturujia inaimarisha nguvu za waamini kumhubiri Kristo; na kwa njia hiyo inawaonyesha wale walio nje (nalo) Kanisa lililo ishara iliyoinuliwa juu kati ya mataifa, ambayo chini yake watoto wa Mungu waliotawanyika wakusanyika katika umoja, mpaka liwapo zizi moja na mchungaji mmoja (SC 2).

Asili ya neno liturujia ni maneno mawili ya kigiriki
Laos = watu ergon = kazi.
Hivyo neno hilo lilikuwa likitumika kuonyesha


Lakini Biblia ya Kigiriki (OT) ilitumia neno liturujia kumaanisha:

Katika Agano Jipya limetumika mara 15 kumaanisha


Katika mafundisho / maandishi ya Kanisa
    Kadiri ya Mediator Dei iliyotolewa na Papa Pius XII, Nov. 20, 1947.


Ni adhimisho la hadhara ambamo, Kristo Mkombozi wetu anamtukuza Mungu Baba; pia ni adhimisho la hadhara ambamo Kanisa linamtukuza Kristo, mwanzilishi wake; na kwa njia yake, pamoja naye na ndani yake, Kanisa linamtukuza Mungu Baba. Kifupi ni tendo la kumtukuza Mungu lifanywalo na Mwili wote wa fumbo, yaani Kichwa na mwili.

Hivyo:


    Kadiri ya Sacrosanctum Concilium (Des. 4, 1963)


Ni utekelezaji wa kazi ya kikuhani ya Yesu Kristo. Katika Liturujia, kwa ishara zinazoonekana, huonyeshwa na kutendeka kutakatifuzwa kwake binadamu, kila ishara ikiwa na maana ya pekee. Katika Liturujia, ibada halisi za hadhara huadhimishwa na Mwili wa fumbo wa Yesu Kristo, yaani na Kichwa na viungo vyake.
Kwa hiyo kila adhimisho la kiliturujia, kwa kuwa ni tendo la Yesu Kristo Kuhani na la Mwili wake, ndilo Kanisa, ni tendo takatifu kupita yote na hakuna tendo jingine la Kanisa linalofanana nalo kwa manufaa kwa kiwango kile kile na kwa daraja ile ile (SC 7).

Hivyo:


    Asili ya liturujia ya Kanisa


Mtaguso wa II wa Vatican unaeleza kuwa liturujia, ambayo yaweza pia kuelezwa kuwa ni mkutano kati ya mtu na Mungu katika Kristo, ndani ya Kanisa katika alama takatifu, ni tendo la hali ya juu sana, na hasa ni kilele cha maisha ya ukristo. Katika kusherehekea mafumbo ya liturujia tunamtukuza Mungu kadiri Mungu mwenyewe anavyotaka. Hivyo inaweza kuelezwa kuwa liturujia:

Mungu Baba (Liturgy is Theocentric):

Kiini cha liturujia ni Mungu mwenyewe
Mkutano huo kati ya Mungu na mtu ni mkutano kati ya pande mbili zisizo sawa. Ni kati ya Muumba na kiumbe; kati ya Mungu mkamilifu na mtu ambaye anamtegemea Mungu kwa kila kitu. Mungu ndiye anayeanzisha / anayeitisha mkutano huo.

Lengo la liturujia ni utukufu kwa Mungu. Maisha ya binadamu lazima yaelekezwe kumjua Muumba wake. Agano kati ya Mungu na Mwanadamu ni kati ya pande zisizo sawa: Udogo huu wa binadamu mbele ya Mungu huonyeshwa kwa namna binadamu anavyotakiwa kujinyenyekesha mbele ya Mungu kwa kumsifu, kumwomba, n.k.

Mungu Mwana ametukomboa:
Katika liturujia tunakutana na Mungu Baba kwa njia ya Yesu Kristo katika Roho Mtakatifu. Kristo yupo katika maadhimisho ya liturujia yetu kwa namna mbali mbali: Katika Neno lake, Sakramenti, Mwili na Damu, Watumishi na mkutano wa kidini. Kwa namna ya pekee, kwa fumbo la Pasaka Kristo anatupatanisha tena ulimwengu na Mungu. Rejea: Worship in time and space.

Roho Mtakatifu:
Hakuna awezaye kusema kuwa Kristo ni Bwana ila kwa nguvu ya Roho Mtakatifu (IKor 12:3). Ndiye anayetufundisha na kutukumbusha yote aliyosema Kristo (Yoh 14:26). Kwa leo tunatia nanga sehemu hii ya kwanza ya tafakari kuhusu maana ya Liturujia kama inavyochambuliwa kwako na Askofu Salutaris Melchior Libena wa Jimbo Katoliki Ifakara na Mwenyekiti wa Idara ya Liturujia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.








All the contents on this site are copyrighted ©.