2013-11-30 14:58:38

Bwana Rolando Marranci ateuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Vatican


Baraza kuu la Benki kuu ya Vatican limemchagua Bwana Rolando Marranci kuwa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Vatican, uteuzi huu unaanza rasmi tarehe 30 Novemba 2013.

Itakumbukwa kwamba, kabla ya uteuzi huu, Bwana Marranci alikuwa ni mkurugenzi msaidizi wa Benki ya Vatican; uteuzi uliokuwa umefanywa hapo tarehe 1 Julai 2013 na kuridhiwa na Baraza kuu la Benki ya Vatican linaloundwa na Tume ya Makardinali.







All the contents on this site are copyrighted ©.