Mkristu huelekeza njia zake za mawazo kwa Mungu, na kukataa mawazo dhaifu yanayotaka
kumweka mbali na Mungu. Ilikuwa kiini cha mahubiri ya Papa Francisko mapema Ijumaa,
wakati wa Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta. Papa alizungumzia
juu ya mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake juu ya kuzielewa dalili za nyakati akisema,
Mkristu anapaswa kufikiri si kwa akili yake tu lakini kwa muono wa ndani wa moyo na
kiroho. Na Mkristu, kufikiri kwa kuongozwa na Mungu ina maanisha , kukataa mawazo
dhaifu yenye kuelekea katika kutenda dhambi. Papa Francisko ameendelea kufundisha
akirejea somo la Injili ambamo Bwana aliwafundisha wanafunzi wake kuzielewa dalili
za nyakati , na ishara ambazo Mafarisayo hakuzifahamu. Amesema Wale ambao humfuata
Yesu, si tu hufikiri kwa vichwa vyao, lakini pia kwa moyo na roho ndani, vinginevyo
ni vigumu kuielewa njia ya Mungu katika historia.
Akirejea somo la Injili
ya siku ambalo linazungumzia wanafunzi wawili wa Emmaus kukutana na Yesu, Papa alisema,
si kwamba Yesu alikuwa na hasira kiasi hicho lakini alijifanya hivyo, wakati Wanafunzi
wake waliposhindwa kuelewa mambo. Aliwaita wajinga, na wenye mioyo mizito , wasio
elewa mambo ya Mungu na mwana wa mtu. Papa anasema, hata kwetu leo hii, Bwana
anatukemea kwa kutoelewa nini kinatokea katika maisha yetu, na hasa maisha binafsi
, kile kinachotokea ndani ya moyo na kile kinachotokea katika ulimwengu , katika
historia na kwa wakati huu. Papa ameziita hizi ni dalili za nyakati ! Kumbe , roho
ya ulimwengu hutupa sisi mawazo mengine, kwa sababu roho wa ulimwengu hana mapenzi
na watu, anapenda kuwaingiza wengi katika mtengo huu wa malimwengu wa bila kuwapa
uhuru wa kuwaza vyema.
Roho wa ulimwengu, anayeshinikiza wote watembelee
katika njia hiyo ya maovu , lakini kama alivyonya Mtume Paul, roho wa ulimwengu atatupeleka
iwapo tu hatuna uwezo wa kufikiri juu yetu wenyewe, anaweza kutupeleka kasi,kama wasiokuwa
huru.
Papa aliendelea kuzungumzia juu ya uhuru wa kufikiri akisema kwamba,
ni kufikiri kwa uhuru, kwa lengo la kuelewa nini kinatokea. Lakini Binadamu peke yake
hawezi. Anahitaji msaada wa Bwana. Tunahitaji kuelewa dalili za nyakati, na Roho
Mtakatifu anatupa zawadi hii , zawadi ya akili ya kuelewa, si kwa sababu wengine
wanasema nini kitatokea lakini ni uelewa wa ndani wa mtu mwenyewe.
Papa katika
homilia hii, ametoa mwaliko kwa wote wanaotembea katika njia hii ya imani kujiuliza,
Bwana anataka ni nini? Kuomba daima roho wa akili wa kuelewa dalili za nyakati. Kumwomba
Yesu kwa neema hii, ili tupate na kumtumia roho wa akili, kukabiliana na mawazo dhaifu,
yenye kuondoa ufahamu huu na kutuweka mbali na Mungu. Tuombe zawadi hii ya Roho wa
akili katika kutafuta nini maana mambo na katika kuzielewa ishara za nyakati. Alihitimisha
, tunaomba ni neema ya Bwana , tukiwa tumejawa na imani kwamba, Yeye ana uwezo wa
kutupa Roho wa akili na kuelewa ishara za nyakati.