Serikali ya Saud Arabia imewafukuza wahamiaji 40, 000 kutoka Ethiopia waliokuwa wanaishi
nchini humo kinyume cha sheria tangu mapema Mwezi Novemba, 2013. Serikali imetoa vibali
vya kuishi na kufanya kazi nchini humo kwa wahamiaji millioni 4 kutoka sehemu mbali
mbali za dunia.
Hayo yamebainishwa na Bi Dina Mufti, Balozi wa Ethiopia nchini
Saud Arabia. Hadi kukamilika kwa zoezi hizi, zaidi ya wahamiaji 80, 000 watakuwa wamerudishwa
nchini Ethiopia. Takwimu zinaonesha kwamba, sehemu kubwa ya wahamiaji hawa ni wanawake
wanaofanyishwa kazi za nyumbani nchini Saud Arabia na wakati mwingi wanaishi katika
mazingira hatarishi.
Taarifa za Serikali ya Ethiopia zinaonesha kwamba, Saud
Arabia bado ina uhusiano mzuri na Ethiopia na kwamba, zoezi hizi halitaathiri uhusiano
wa kidugu baina ya nchi hizi mbili.