Nyumba 185, 000 kujengwa kwa ajili ya wananchi wenye kipato cha chini
Rais Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia ametangaza mpango mkakati wa ujenzi wa nyumba
nafuu zipatazo 185,000 ili kuhakikisha kwamba, wananchi wa Namibia wanaishi katika
makazi bora zaidi. Ujenzi huu unakwenda sanjari na huduma ya maji safi na salama pamoja
na umeme.
Mkakati huu unawalenga zaidi wananchi wenye kipato cha chini Namibia
ili hatimaye, kuondokana na makazi yasiyo rasmi yanayopaswa kubomolewa kwenye maeneo
ya mijini nchini Namibia. Mpango huu unalenga kujenga wastani wa nyumba 12, 000 kila
mwaka na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mwaka 2030 kwa gharama ya billioni 4 na nusu
za Marekani.