2013-11-28 14:02:40

Monsinyo Alfred Xuareb kusimamia mchakato wa mabadiliko Benki ya Vatican


Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Alfred Xuereb kuwa mwakilishi wake katika Tume ya Kipapa inayohusika na Benki ya Vatican na Tume ya Kipapa ya Mabadiliko ya shughuli za Benki ya Vatican na masuala yote ya uchumi wa Vatican.

Atakuwa na wajibu wa kuangalia kwa ukaribu mwenendo wa tume hizi na kumpatia taarifa, kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Vatican kuhusu hatua muhimu ambazo atapaswa kuzichukua kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.







All the contents on this site are copyrighted ©.