2013-11-28 15:08:59

Kuzungumza na watu wa imani zingine si ujanja wa kuwaongoa wengine lakini ni kuelimishana.


Mazungumzo na dini zingine haina maana ya kukana imani, wala si kuiongokea dini nyingine, lakini ni kupeana ufahamu zaidi juu ya imani na maadili na kile anachosadiki mwingine. Papa Francisko, aliwaasa washiriki wa Kikao cha Baraza la Kipapa kwa ajili ya majadiliano ya kidini, hapa Vatican.
Amesema, kinyume chake, kama alivyo onya katika waraka wake wa Furaha ya kuinjilisha, "Evangelii Gaudium" ni kuwa na majadiliano ya dhati na kwa moyo wa ukweli na furaha ya kuifunua imani kwa mtu mwingine . Ni nafasi ya kuuzamisha utambulisho wa dini kwa uwazi wenye uwezo wa kuweza kujenga mahusiano ya kibinadamu, kati ya wanaoamini na wasioamini.

Majadiliano kama fursa ya kukua katika udugu , utajiri wa ufahamu na utoaji wa shuhuda. Kwa sababu hii Papa amesema, mazungumzo kati ya dini na uinjilisha hakuna tofauti. Na wala si suala ya kulazimisha imani yoyote kwa nguvu, wala si kutumia mikakati ya ujanja wa kuwavutia wengine kwa nguvu, lakini badala yake, ni utoaji wa ushahuda kwa furaha na unyenyekevu unaoonyesha ukomavu katika katika tumaini na a kuajianimi
Kama wafuasi wa Yesu. - aliongeza , sisi lazima kujitahidi kuondokana na hofu , daima tayari kupiga hatua ya kwanza kuingia katika majadiliano haya , bila kukata tamaa wala soga wa katika kukabiliana changamoto na matatizo, na kutoeleweka yanayoweza kujitokeza.








All the contents on this site are copyrighted ©.