2013-11-27 16:22:37

Furaha ya Injili hujaa katika mioyo ya wanaokutana na kuishi na Yesu


Watu mbalimbali wanaendelea kutoa maoni yao juu ya Waraka wa Kwanza wa Kitume wa Papa Francisko "Wenye jina: Furahi ya Injili (Evangelii Gaudium) ambamo ameanza na ujumbe kwamba, Furaha ya Injili hujaa moyoni na katika maisha ya wale wanaokutana na Yesu.

Papa Francisko katika waraka huu anazungumzia mandhari ya kutangaza Injili katika dunia ya leo na miongoni mwa mambo mengine, ameutazama kwa makini mchango wa Sinodi ya Maaskofu iliofanyika hapa Vatican kwa Kaulimbiu : Uinjilishaji Mpya kwa ajili ya kuieneza Imani, iliyofanyika Vatican, Oktoba 7 hadi 28 , 2012. Aidha wachambuzi, mmoja wao akiwa Sergio Centofatti wanasema, pia Waraka huu ni muhimu kwa utume wa Kanisa. Na unao nyesha mwelekeo wa njia ya Kanisa katika miaka ijayo.

Wachambuzi hao wameyatenga yaliyoandikwa katika waraka huu wwenye kurasa 224, katika mafungu matano ifuatavyo:
1.Uinjilishaji Mpya
Waraka unalenga kuzindua hatua mpya ya uinjilishaji wenye sifa ya kuwa na furaha katika kuinjlisha . Na ni wito wa dhati kwa wakabatizwa wote, kuwa na mapenzi ya kuinjilisha, kwa sababu mapenzi ya kufanya hivyo , yanatia nguvu katika kuwa na mabadiliko ya maisha yenye kuwavutia wengine katika upendo wa Yesu, kama sehemu ya uzoefu wa maisha yao, furaha na uzuri wa urafiki na Yesu , katika hali ya kudumu . Wakristo wameitwa kuwa wainjilishaji kwa roho moja ya uchaji na utendaji , wa kutangazai Injili “kerygma " kwamba Yesu Kristo anakupenda, alitoa maisha yake ili kuwaokoa, na sasa yu hai na yukio karibu nawe kila siku, akikuangazia, kukupa ujasiri na kuweka huru dhidi ya dhambi.
2.Maadiliko mapya, Ubunifu na umahiri
Upya, ubunifu na umahiri , unaotokana na kurudia kusoma upya Injili, ni sharti kwa Wachungaji na wale wote wanaofanya kazi za kitume kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika miundo, kwa kuwa katika kanisa, wote ni wamisionari . Mabadiliko haya si Parokiani au majimboni tu lakini hata katika utawala wa kiti cha Petro, kunahitajika uongofu mpya kwa ajili ya kutembea pamoja katika barbara ya ushirikiano na mshikamano zaidi.Papa anasisitiza haja ya kuongeza jukumu kwa walei, na kupanua uringo kwa ajili ya uwepo zaidi nafasi zaidi za utendaji wa wanawake katika Kanisa, hasa katika maeneo ambapo wanawake huwa na nafasi ya kusikilizwa katika utoaji wa maamuzi .

3.Kanisa lililo wazi, karimu na huruma.
Waraka wa Papa katika hili unalitaka kanisa kuwa wazi. Kanisa lililo tayari kumpoeka kila mtu tena kwa moyo wa huruma na si kuhukumu, kwa sababu Mungu kamwe hachoki kusamehe. Papa anahimiza waamini kutofungiwa milango ya Sakramenti, hata kwa sababu nyepesi. Ameitaja Ekaristi kuwa si tuzo lakini ni ukarimu na chakula cha Bwana cha wanyonge . Amewataka Wachugaji kutumia busara na ujasiri katika utendaji waowa kichungaji ili kila mmoja ajisikie kupendwa na kanis alicha ya madhaifu yake.
Na kwamba kumtangaza Kristu kwa wale wasiokuwa na urafiki na Yesu, ni muhimu na lazima kuwa na sifa chanya za ukarimu, heshima , huruma na uvumilivu bila ya kuchoka katika safari hii ndefu nangumu. Katika hili Papa pia ametaja mahubiri ya mapadre ni lazima yaonyesha neema hii ya matumiani ya yasiyo kuw ana ukomo, kutolewa daima kwa unyenyekevu na huruma lakini kwa maneno yenye kupenya mioyo.

4Mahusiano ya karibu kupitia njia ya kukutana na kujadiliana.
Na Majadiliano na kukutana na Wakristu wengine (Uekumene ), ni njia muhimu ya uinjilishaji, kama ilivyo pia katika kukutana na dini zingine na wasio amani. HIli pia ni sharti muhimu kwa Mkatoliki katika kueneza imani na amani. Mazungumzo ni lazima yafanyike katika hali ya uwazi na furaha isiyokuwa na uficho katika uinjilishaji. Hasa, Papa alibainisha kuwa " katika hili umuhimu utolewa zaidi katika kujenga mahusiano na waamini Waislamu. Papa Francisko ameombahili lifanyike kwa unyenyekevu na uvumilivu wote, hasa katika mataifa ya mapokeo ya Kiislamu kwa ajili ya kurejesha dhamana uhuru wa dini kwa Wakristo, kama waumini wa Kiislamu wanavyo furahia uhuru huo katika nchi za Magharibi.

5. Kanisa daima sauti ya kinabii.
Kanisa ni sauti ya kinabii, yenye kuwa na uwezo wa kusema kwa sauti ya ujasiri... hata dhidi mwelekeo pinzani wa kijamii. Papa amelitangaza Kanisa, kuw ani Kanis aMaskini ka ajili ya Maskini. Hivyo Papa ametoa wito kwa Kanisa maskini kuwa huduma ya maskini. Papa anakemea mifumo ya sasa ya kiuchumi kwamba, haki imefunikwa na utendaji wa mimi kwanza. Na amerejea hali za maisha ya watu masikini waliotupwa pembezopni na jamii na watoto ambao hawajazaliwa , na asili ya muundo wa familia ya binadamu kuvurugwa, mateso na madhulumu kwa makundi manyonge ya watu, akisema Kanisa linaakiwa kuwa mstari wa mbele kuwatetea wote hao.








All the contents on this site are copyrighted ©.