Pamoja na mvutano mkubwa wa kisiasa , Mons. Martinelli bado anaaamini uwepo wa mwanya
wa amani-Libya
Shinikizo kali linaloendelea kwa ajili ya kufanikisha maridhiano
ya kijamii, kwa hakika ni jambo jema, na lenye kuleta tumaini kwa Libya kuweza kupata
tena hali ya utulivu na amani wakati wowote. Ni maelezo ya Askofu Mkuu Giovanni Innocenzo
Martinelli , Mwakilishi wa Kitume, Tripoli , Libya, wakati akizungumza na shirika
la habari la Fides.
AskofuMkuu Martinelli anasema, iwe katika mji wa Benghazi
au kwa Tripoli kuna shinikizo kubwa kwa sababu makundi mbalimbali ya wanamgambo wanaofanya
udhibiti katika miji hiyo miwili , wameanza kuweka silaha chini na kuruhusu vikosi
vya usalama vya serikali kufanya shughuli zake.
Na kwamba Maandamano ya Novemba
15, karibu na makao makuu ya Tripoli yaliyofanywa na wanamgambo kutoka Misrata, yalichochewa
na ufyatuaji wa risasi na kusababisha vifo 46 na zaidi ya 500 kujeruhiwa. Baada ya
hilo, wakazi wa jiji hilo waliingia mitaani kuonyesha uvumilivu wao kwa uwepo wa makundi
ya watu wa kawaida wenye kuwa na silaha. Hata katika Benghazi baada ya mapigano ya
Jumapili , kati ya jeshi na wanamgambo wa Kiislam, yaliyo sababisha vifo 9 na 51 kujeruhiwa,
Mamlaka ya mji huo Jumatatu, yaliruhusu maandamano ya amani mitaani kupinga hilo.
Na
kwamba maisha katika jiji la Tripoli, sasa yako katika kipeo cha juu cha mivutano
pia kama ilivyo katika mji wa Beghazi ambapo amebaki Mwakilishi w Kitume Mons Magro,
na baadhi ya wafanyakazi wachache katika taasisi za kikanisa ameeleza Mons. Martinelli
. Akireje ahali hiyo anasmea kwa wakati huu , kanisa haliwezi kufanya mengi kuhusu
kazi za kitume na kichungaji kwa jumuiya ndogo Katoliki, ambayo nayo inazidi kupungua
siku hadi siku , na hasa baada ya Masista kuondoka kwa hofu za kushambulliwa na hivyo
wamebaki wauguzi wachache ambao wanaendelea kutoa msaada na huduma ya thamani, katika
hospitalini. Mons. Martinelli amekiri kwamba, wanaunaishi wakati mgumu na wenye
uchungu. Ni kitendawili cha Libya kinachohitaji kufumbuliwa , na bado kuna tumaini
kwamba Walibya ipo siku wataweza kupatana na kuishi kwa amani.