2013-11-25 11:00:16

Wafadhili wasitisha misaada kwa Malawi kutokana na rushwa na ufisadi!


Serikali ya Malawi imepinga vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Umoja wa Ulaya, Uingereza, Norway pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, kwa kushindwa kusimama kidete kupambana na rushwa, ufisadi pamoja na ubadhirifu wa mali ya umma nchini Malawi.

Bwana Brown Mpinganjira, Waziri wa habari anasema, anashindwa kuelewa lengo la vikwazo hivi kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kusitisha kutoa misaada ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya wananchi wa Malawi!







All the contents on this site are copyrighted ©.