2013-11-25 10:32:43

Siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake!


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, iliyoanzishwa kunako mwaka 2008 anawataka wadau mbali mbali kuhakikisha kwamba, wanashiriki kikamilifu kulinda na kutetea haki msingi za wanawake na wasichana.

Anawapongeza wakuu wa Serikali wanaosaidia mchakato wa kubadilisha mtazamo wa watu pamoja na mashujaa ambao wamesimama kidete kulinda na kutetea haki msingi za wanawake bila woga kama ilivyo kwa Denis Mukwege, muasisi wa Hospitali ya Panzi iliyoko nchini DRC. Hii ni hospitali ambayo inatoa msaada wa matibabu kwa wanawake wanaokabiliwa na nyanyaso za kijinsia nchini DRC. Dr. Mukwege anapaswa kuwa ni mfano a kuigwa katika kuwahudumia wanawake sehemu mbali mbali za maisha ya kijamii.

Jumuiya ya Kimataifa kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba 2013, itakuwa inaendesha kampeni dhidi ya vitendo vya nyanyaso kwa wanawake na wasichana sehemu mbali mbali za dunia. Umoja wa Mataifa unawataka watu kuchangia kwa hali na mali katika kufanikisha kampeni hii, ili hatimaye, kuwalinda pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa kiuchumi ili waweze kujitegemea.







All the contents on this site are copyrighted ©.