2013-11-25 13:55:33

Rais wa Paraguay akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 25 Novemba 2013 amekutana na kuzungumza na Rais Horacio Manuel Cartes Jara kutoka Jamhuri ya Watu wa Paraguay, ambaye pia amekutana na viongozi waandamizi kutoka Vatican chini ya Askofu mkuu Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamepongeza uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili. Baadaye amejadili kwa kina na mapana kuhusu hali halisi ya maisha ya wananchi wa Paraguay na Amerika ya Kusini katika ujumla wake; mapambano dhidi ya umaskini, rushwa na ufisadi pamoja na mikakati inayopania kumwendeleza mtu mzima: kiroho na kimwili sanjari na haki msingi za binadamu! Wamejadili pia mchango wa Kanisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wa Paraguay. Kwa pamoja wameonesha utashi wa nchi hizi mbili kushirikiana zaidi katika ngazi ya kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.