Kukamilika kwa mwaka wa Imani, ni mwaliko wa majitoleo zaidi katika imani, maoni
ya Salvatore Martinez.
Mwaka wa Imani uliozinduliwa na Papa Mstaafu Bendikto XV1, Octoba 2012 na kuhitimishwa
na Papa Francisko, Jumapili 24 Novemba, umekuwa wa kipekee uliojaa lafudhi na utendaji
mbalimbali wa kanisa katika umoja wa imani, ulioweka ujumbe wa Injili, kuwa kiini
cha utendaji wote wa kanisa. Ni Maoni ya Rais wa Kitaifa wa Uhuisho wa Kiroho hapa
Italy , Bwana Salvatore Martinez, akiutafakari mwaka wa Imani. Katika mahojiano
na Mwanahabari Federico Pianni, Martinez amekitaja kipindi cha mwaka mzima wa imani
kwamba, kimekuwa ni kipindi kilicho leta mwamko kwa wengi kutazama hali halisi za
imani katika maisha ya wengi. Wengi wanakubali kwamba imani imedhoofika kwa waaamini
wengi. Wengi wamebaki katika hali ya uvuguvugu. Na hali hiyo inaleta haja ya kutamfuta
mbinu mpya za kuimarisha imani , kutoa ufahamu zaidi kwa njia mbalimbali, ikiwemo
kusoma na kutafakari upya imani, na historia ya Neno la Mungu kumwilishwa. Kuona
kwa jinsi gani mtu bado anaweza kukombolewa na Injili na Kanisa kuumwilishi upendo
wa Injili katika utendaji wake wote wa ubinadamu. Na hivyo, Martinez anaendelea
kusema, Papa Benedikto XVI, aliona haja ya kuweka katika kalenda ya Kanisa mwaka
wa Imani, kama juhudi za kuufufua upya, yaliyo azimiwa na Kanisa katika maadhimisho
ya mwaka Mtakatifu 2000. Na kujiuzuru ghafla Papa Benedikto katika utume wa kuliongoza
Kanisa kama Papa, baada ya kuutangaza mwaka wa imani , kwa wengi kumetoa fundisho
kubwa, hasa kwa waamini kusikiliza na kutenda kwa kadri sauti ya ndani inavyosema.
Maamuzi ya kustaafu Papa Benedikto XV1, yameonekana kuwa kweli si maamuzi yake binafsi
bali yalitoka kwa Roho Mtakatifu ambaye ni yuleyule aliyemweka katika nafasi yake
Papa Francisko, anayeendelea kuonyesha ishara ya ukuu wa Papa duniani, kwa ajili
ya Injili, na Kanisa la ulimwengu. Kanisa ambalo daima liko karibu na watu. Ukaribu
unaotoa uelewa mpya zaidi wa maana ya Kanisa , kuwa ni upendo kwa watu wote. Ni upendo
wa kmajitoleo ya kujibakiza na kuwa sadaka kwa ajili ya wengine.
Salvatore
Martinez, alieleza huku akiangalisha pia katika malengo ya Kanisa baada ya mwaka
wa imani, kama ilivyo ainishwa na Papa kwamba, lengo la kwanza kuendelea kuitangaza
Imani kwa nguvu pande zote,za dunia bila kupunguza kitu , na kufanya uzuri wote
wa Injili na ukweli wake uonekane kwa watu wote kama ilivyoandikwa katika waraka
wa Lumen Fidei ... Lengo la pili ni waamini kuendelea kuihuisha upya imani, katika
nyakati hizi za mabadiliko ya mifumo mipya ya maisha yanayo lenga kudhoofisha imani.
Ni kuihuisha upya imani, kujikabidhi kwa Bwana wa Injili, kama tunayemkiri katika
imani. Lengo la tatu ni kutafuta jinsi watu wanavyoweza kurudisha imani yao kwa
Kanisa. Kusema ndiyo kwa Kanisa, kwa sababu kwa wakati huu watu wengi wanaonyesha
kuwa na imani kwa Yesu, lakini hawana imani na kanisa. Mwaka wa Imani imekuwa ni
kipindi cha kusema ndiyo kwa Kanisa. Na hiyo ina maana ya kutambua kwamba, imani
hii ni msingi wake umo katika mwili wa kanisa. Pamoja na malengo hayo, kuna changamoto
zilizo ainishwa Papa Francisko. . Kwanza ni jinsi ya kuleta mabadiliko mapya katika
mifumo ya utendaji wa Kanisa na taasisi zake . Pili ni jinsi ya kufanikisha Uinjilishaji
mpya, katika maana ya kuwa na uwazi zaidi kulingana na mahitaji ya nyakati zetu, dhamira
kubwa kwa watendaji wa kanisa hasa wachungaji, ma wanapo fanya kazi ndani ya Kanisa,
na pia kwa kila muumini, matendo yao yaweze kuushuhudia upendo wa Injili. Aidha kuna
changamoto kwa viongozi kuwaongoza watu kwa upendo wa kina na huruma. Upendo na huruma,
wakiiona kuwa ni kuwa ni zawadi ya imani itokayo kwa Mungu yenye kushukia kila muumini.
Na hivyo, changamoto hii ni kwa kila Padre kigangoni parokiani na kusambaa hadi kitaifa
na kimataifa.