2013-11-25 07:47:18

Kongamano la dawa asilia kufanyika Jijini Kampala, Uganda, Julai 2014


Mfuko wa Msamaria Mwema ulioanzishwa na Mwenyeheri Yohane Paulo wa Pili, unaoendeshwa na kusimamiwa na Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa wafanyakazi katika sekta ya afya, Jumatatu tarehe 25 Novemba 2013, unafanya mkutano kuhusu Mradi wa Afrika unaojulikana kama "Africae Munus", kama njia ya kuunda mtandao wa vyuo vikuu kutoka Barani Afrika, ili kushirikishana utajiri wa ujuzi, rasilimali, miradi na malengo mbali mbali mintarafu Mafundisho ya Mababa wa Kanisa.

Mradi huu ulizinduliwa Mwaka 2012 na kwa sasa unavishirikisha vitivyo vya afya kutoka: DRC, Msumbiji, Chad, Burkina Faso, Tanzania na Uganda. Mkutano huu pamoja na mambo mengine unachambua mafanikio yaliyokwisha kupatikana katika kipindi cha mwaka mmoja ili kuweka mikakati inayotakiwa kutekelezwa kwa siku za usoni. Lengo ni kusaidia kujenga uwezo wa Kanisa Barani Afrika kuwaandaa mabingwa katika sekta ya afya, kwa kushirikiana na vyuo vikuu Barani Ulaya, Amerika ya Kusini na Canada.

Mkutano huu unazungumzia pia kongamano la kimataifa litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, mwishoni mwa Mwezi Julai 2014 ili kujadili kuhusu Dawa Asilia.







All the contents on this site are copyrighted ©.