2013-11-24 15:17:03

Sala ya Kanisa kwa mahitaji ya watu mbali mbali!


Katika Sala ya Waamini iliyotolewa kwa lugha mbali mbali, waamini katika kuliombea Kanisa kwa ujumla, wamemwomba Kristo, kichwa na mchumba wa Kanisa aliyejitoa kwenye Altare ya Msalaba, kuwalinda katika imani; kuwaimarisha matumaini na kuwaenzi katika mapendo.

Sala kwa ajili ya Makleri na Wainjilishaji, waamini wamemwomba Kristo, sura ya Mungu asiyeonekana, aliyemfunulia mwanadamu uso wa Baba yake wa mbinguni, awabariki, awalinde na kufanikisha jitihada zao.

Sala ya waamini kwa ajili ya watu wote duniani pamoja na viongozi wao, Kanisa limemwomba Kristo Mfalme wa mbingu na dunia kuwasaidia watu wa mataifa kushinda chuki na maovu, ili hatimaye, kuwafungulia njia ya msamaha na amani kwa wote.

Mama Kanisa amewakumbuka na kuwaombea wadhambi na wote wasio amini, ili kwamba Kristo ambaye ni utimilifu wa nguvu na mamlaka yote, aweze kuziangazia akili na mioyo yao kwa njia ya toba na kuwasafisha kwa huruma yake.

Katika maombi, Kanisa limeendelea kuzikumbatia familia, maskini na wapweke, ili Kristo mzaliwa wa kwanza katika viumbe vyote aweze kuwapatanisha, kuwafariji pamoja na kuwaondolea taabu na mahangaiko yao ya ndani, ili waonje furaha ya kweli!








All the contents on this site are copyrighted ©.