Mkutano juu ya Mabadiliko ya tabia nchi: viongozi fikirieni leo na kesho
Jumatatu19 Novemba 2013, Mkutano wa Kimataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi (COP
19) ulioanza wiki iliyopita na vikao vya tume tendaji, , ulifunguliwa rasmi mjini
Warsaw Poland na kuhudhiriwa na wakuu wa nchi kadhaa, wajumbe wawakilishi wa makampuni
na mashirika na viwanda, vyombo vya habari na taasisi za utafiti. Lengo la Mkutano
huu wa wiki mbili, unaokamilika 22 Novemba 2013, ni kukutanisha watalaam toka mataifa
mbalimbali, ili washrikisha utajiri wa ufahamu na uzoefu katika masuala yanayo gandamiza
uchumi, na uwepo wa mabadiliko katika tabia nchi. Na pia kujadili dharura zinazo
tajwa na jumuiya ya kisayansi , katika hoja ya binadamu kuwa makini na utendaji wake.
Mkutano huu ni ufuatiliaji wa majadiliano yanayo lenga katika kukamilika kwa
Malengo ya mwaka 2015, na makubaliano ya kimataifa yanayo lenga malengo ya COP21,
yatakayo fanyika mjini Paris , lkama ilivyo kubalika mwaka jana katika mkutnao wa
COP18 Doha, Qatar. Majadiliano ya mjini Paris, yanatazamiwa kutengeneza utekelezaji
hadi 2020 wakati ambapo wengi wataweza kushuhudia maana ya lengo la kupunguza ongezeko
la joto duniani kwa nyuzi joto mbili nje, ambalo limeshndikana kufikiwa.
Tume
ya Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Hewa, UNFCCCC, katika tamko lake la Jumatatu
, wakati wa kuanza rasmi mkutano wa COP 19 mjini Warsaw, limetoa wito kwa serikali
ya kuunganisha utendaji wa nguvu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa katika ngazi
zote za utendaji wa serikali na jamii na kufanya maendeleo halisi, kuelekea mafanikio
katika mkataba wa Kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, kwa mwaka 2015.
Rais
mpya aliyechaguliwa na Mkutano wa Wanachama (COP 19/CMP9 ), Mheshimiwa Marcin Korolec,
Waziri wa Mazingira Poland, katika hotuba yake ya ufunguzi, ameeleza kuwa, mabadiliko
ya tabia nchi ni tatizo la kimataifa, ambalo ni lazima kulifanya lipige “about turn”.
Ni tatizo kama hatuwezi kuratibu vitendo vyetu, na lazima kutenda kwa ushirikiano.
Utendaji wa nchi moja au kikundi kimoja kimoja hakuwezi kusitisha tatizo. Na ni sisi
binadamu tunaotakiwa kuungana na kutenda kwa mshikamano mmoja, ili kulinda vizazi
vya sasa na ya baadaye.