Kuna haja ya kulinda na kudumisha heshima ya kazi na utu wa wafanyakazi!
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 18 Novemba 2013 amekutana na kuzungumza
na Bwana Guy Ryder, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kazi Duniani, ILO, ambaye amesema
kwamba, Kanisa na Shirika lake linakazia umuhimu wa kulinda na kudumisha heshima ya
kazi na utu wa wafanyakazi, hasa wale wanaotekeleza majukumu yao katika mazingira
hatarishi.
Viongozi hawa wawili wanasikitishwa sana na ongezeko la biashara
haramu ya binadamu inayoendelea kuwatumbukiza wanawake na wasichana katika utumwa
mamboleo. Kazi yenye hadhi na utu wa binadamu ni kati ya mambo msingi yanayotarajiwa
kutekelezwa na Jumuiya ya Kimataifa baada ya kukamilika kwa Malengo ya Maendeleo ya
Millenia kwa Mwaka 2015.
Shirika la Kazi Duniani, linashirikiana kwa karibu
zaidi na Taasisi za Kanisa Katoliki na kwa namna ya pekee na Baraza la Kipapa la haki
na amani katika mchakato wa kuhakikisha kwamba, haki jamii inazingatiwa na wengi.
Bwana Ryder amekutana na kuzungumza pia na viongozi wa Serikali ya Italia pamoja na
vyama vya kiraia