2013-11-16 08:53:39

Manila, Siku ya Maombolezo na Matumaini!


Kardinali Luis Antonio Tagle, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Manila, Ufilippini, anawalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema, Jumamosi tarehe 16 Novemba 2013 kufunga na kusali kama alama ya mshimkamano wa dhati na waathirika wa tufani iliyosababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Hii ni siku ya kumlilia Mwenyezi Mungu na kuomba tena fadhila ya matumaini kwa watu wanaoteseka na kuhangaika kutokana na maafa makubwa yaliyowakumba wananchi wa Ufilippini, wanaoteseka na kuomboleza kutokana na kuondokewa na ndugu, jamaa na marafiki zao. Kardinali Tagle, majira ya Saa 2:00 Usiku, ataongoza Sala ya Jioni na Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu, kwenye Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Fernando de Dilao, ambayo kwa sasa inatumika kama makazi ya muda ya Jimbo kuu la Manila, Ufilippini.







All the contents on this site are copyrighted ©.