2013-11-15 10:33:01

Umoja wa Mataifa kushiriki katika maonesho ya Milano 2015


Mashirika 22 ya Umoja wa Mataifa yamejiunga na maonesho ya Expo 2015 yanayoongozwa na kauli mbiu "kulisha dunia, nishati kwa maisha", ili kuimarisha kampeni ya Jumuiya ya Kimataifa katika mapambano dhidi ya baa la njaa na umaskini duniani kwa kuzalisha chakula kitakachotosheleza idadi ya watu billioni 9 ifikapo mwaka 2050. Maonesho haya yatafanyika Milano, Kaskazini mwa Italia kwa miezi sita, kuanzia mwezi Mei hadi mwishoni mwa Mwezi Oktoba 2015.

Umoja wa Mataifa umekuwa wa kwanza katika Jukwaa la Kimataifa kujiunga na hatimaye, kutia sahihi mkataba wa maonesho haya, kama sehemu ya mchakato wa kupambana na baa la njaa na umaskini, utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ifikapo mwaka 2015. Maonesho haya yanatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya millioni 20 katika kipindi cha Mwaka 2015.







All the contents on this site are copyrighted ©.