2013-11-15 15:45:23

Roho yenye udadisi mwingi huwa na mwelekeo wa kujitenga na Mungu- Papa .


(Vatican Radio) Roho ya udadisi mwingi, huzaa hali kutatanikiwa na ghasia na fujo ya kujiweka mbali na Roho wa hekima , ambaye huleta amani, alieleza Papa Francis katika homilia yake wakati wa Misa Alhamisi asubuhi katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta .

Papa alitoa homilia yake kwa kutafakari masomo ya siku , ambamo somo la kwanza, lilieleza, hali ya kiroho kwa mwanamme na mwanamke, Wakristo wa kweli , wanaoishi katika hekima ya Roho Mtakatifu. Na hekima hii inayowafanya wasonge mbele kwa busara , utakatifu na dhamira safi.

Papa alisema,hii ni safari ya kiroho katika maisha ya kawaida. Na roho hii ni Roho wa Mungu , ambayo husaidia katika utoaji wa hukumu na kufanya maamuzi kulingana na Roho wa Mungu. Ni roho anayetupatia sisi amani daima. Ni Roho ya amani, roho wa upendo , Roho wa udugu na utakatifu halisi. Na hilo ndilo Mungu alilolitaka kwa Ibrahimu, kutembea pamoja nae na kumtegemea, ambako ni kutembea na amani na matumainilicha ya kupambana na hali ngumu na tatanishi. Ni kuufuata utendaji wa Roho wa Mungu anavyosema, na hii hujionyesha katika hekima. Papa aliendelea kusema, mtu mke au mme anayetembea katika njia hii , anakuwa ni mtu mwenye busara, kwa sababu anafuata utendaji wa Mungu katika hali zote, iakishibishwa na Roho wa uvumilivu.

Papa aliligeukia pia somo la Injili na kutahadharisha juu ya binadamu, anaye tafuta roho ya udadisi nyingi , kinyume na hekima ya Mungu. Roho ya udadisi anayetafuta kujikweza katika nafasi za ukuu, nafasi ya kuitwa bwana, na katika kuijua mipango ya Mungu ya baadaye, roho wa kutaka kujua kila kitu na kutaka kuwa na kila kitu mkononi bila kupungukiwa. Ni kama ilivyokuwa kwa Mafarisayo walio mwuliza Yesu ," lini Ufalme wa Mungu utakuja. Ni udadisi wa kutaka kujua hata tarehe siku Mwana wa Mungu atakapokuja. Papa aliizungumzia roho hiyo wa udadisi akionya kwamba, ina hatari ya kujiweka mbali na Mungu, kwa kuwa Mungu hakumfunulia yote Binadamu. .
Papa aliwataka Wakaristu kuwa na udadisi wa kiasi , kusaidia Mkristu kujisikia kwamba, Bwana yu pamoja nae, na si kuendelea kutanga tanga kumtafuta huko na kule.Yesu alisema Ufalme wa Mungu hauji kwa kishindo,wala ufahali, lakini unakuja kwa kwa hekima. Hivo Ufalme wa Mungu tayari uko kati yenu. Alisema Yesu , kwa utambuzi huu wa Roho Mtakatifu , tunapata hekima na amani. Ufalme wa Mungu hauji katika machafuko (ya hali ), kama ilivyokuwa kwa nabii Elia katika upepo na katika dhoruba lakini, katika hali ya utulivu na amani kama upepo mwanana wa utulivu wa hekima.
Papa Francisko anasema, Ufalme wa Mungu hata sasa upo kati yetu, hakuna sababu za kuutafuta katika mambo ya ajabu, au mambo mapya au kwenye udadisi wa kidunia.
Papa Francisko , alimalizia na wito wa kuruhusu Roho wa Mungu, kutuongoza mbele katika hekima , ambayo ni kama upepo mtulivu mwanana. Roho wa Ufalme wa Mungu, ndiye Yesu mwenyewe anayetualika katika ufalme wake.








All the contents on this site are copyrighted ©.