2013-11-15 10:46:11

Jumuiya ya Madola


Rwanda na Msumbiji ni nchi pekee za Jumuiya ya Madola ambazo hazikutawaliwa na Mwingireza, lakini zinashiriki katika mkutano wa Wakuu wa Jumuiya hii unaoendelea mjini Colombo, Sri Lanka. Jumla ya wakuu wa nchi 54 wanachama wa Jumuiya ya Madola wanashiriki, ingawa kuna kinzani kati ya India na Canada wanaoitaka Sri Lanka kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vita na mauaji yaliyojitokeza nchini humo kunako mwaka 2009.

Msimamo kama huu pia umetolewa na Uingereza kwa kuituhumu Sri Lanka kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya wananchi wa Tamil, shutuma ambazo zimetupiliwa mbali na Rais Mahinda Rajapakse wa Sri Lanka.







All the contents on this site are copyrighted ©.