2013-11-15 15:26:56

Italy na Vatican watoa angalisho kwa wimbi la wahamiaji Italia


Alhamis wakati wa ziara ya Papa kutembelea Ikulu ya IItalia "Quirinale" alikuwepo pia Waziri Mkuu wa Italia Enrico letta, akiongozana na Katibu Mkuu wake Phillip Patroni Griff,ambao, baadaye waliutumia muda wao, kukutana na Kaimu Katibu Mkuu wa Vatican Askofu Mkuu Angelo Becciu, na Askofu Mkuu Domenico Mamberti , Katibu wa Vatican katika Mahusiano na Nchi zingine, akiwepo pia Rais wa Baraza la Maaskofu la Italia, Kardinali Angelo Bagnasco.
Mazungumzo ya viongozi hao , yalilenga zaidi suala la uhamiaji, hasa katika mwanga wa majanga ya hivi karibuni, na hali ngumu ya maisha ya wahamiaji na wakimbizi katika kituo cha wakimbizi cha Lampedusa.
Waziri Mkuu wa Italia, alifanya rejea katika kile alichokishudia wakati wa ziara yake huko Lampedusa, ambako Papa Francisko pia alifanya ziara ya kujionea mwenyewe kinachoendelea.
Waziri Mkuu wa Italia , Mheshimiwa Letta katika maelezo yake , aliitumia nafasi hiyo, kutoa taarifa mpya ya kile kinachoendelea katika kituo hicho cha wakimbizi na wahamaiji cha Lampedusa akisema kwamba, serikali yake imechukua hatua mpya za utendaji katika mwambao wa bahari ya Menditterania kwa ajili ya kuzuia maisha ya watu kutumbukia baharini kama ilivyotokea hivi karibuni. Kati ya hatua zilzo imarishwa ni kuwatia mbaroni wote wanao bainika kufanya biashara haramu ya kusafirisha watu kwa vyombo dhaifu baharini, kinyume cha sheria .
Serikali ya Italia na Vatican , kwa pamoja pia katika mazungumzo hayo ya Alhamis, walionyesha kujali kinachoendela Syria na Libya, wakiona kwamba, maafa yanayotokea katika bahari ya Meditterania ni matokeo ya hali za wasiwasi na vurugu za kivita vinavyo shamiri katika mataifa hayo , na hivyo watukuingiwa na wasiwasi wa usalama wa maisha na hivyo kuamua kuondoka bila ya kujali yatakayo kumbana nayo huko wanako elekea. Na hivyo kukuza wimbi wa uhamiaji. Na hivyo, kwa ajili hiyo, Italia na Jimbo Takatifu, wanalitazama tatizo hilo kwa utendaji makini na wa nguvu.








All the contents on this site are copyrighted ©.