2013-11-14 10:58:52

Wananchi Ufilippini wanahitaji msaada wa dharura ili kuokoa maisha!


Mashirika ya Misaada ya Umoja wa Mataifa yanasema kwamba, bado watoa misaada wanakabiliana na vikwazo katika harakati za kuwapelekea waathirika wengi wa tufani iliyoikumba Ufilippini hivi karibuni na kwamba, kiasi cha dolla za kimarekani zipatazo millioni 301 zinahitajika ili kukabiliana na masdhara ya tufani hii ambayo inasemekana kuwa imeacha maafa makubwa kwa wananchi wengi nchini humo.

Zaidi ya watu millioni 10 wameathirika vibaya na wanahitaji msaada wa dharura, kwani kuna mamillioni ya watu wanahitaji: chakula, maji na dawa; baadhi ya wao wameanza kutumia nguvu ili kupata mahitaji haya msingi kutokana na hali ya kukata tamaa na maisha.

Mashirika mbali mbali ya Misaada ya Kanisa Katoliki tayari yameanza kuelekeza nguvu zake nchini Ufilippini na kwamba, walengwa wakubwa ni wale walioathirika zaidi katika maeneo ya Visayas ambako kuna watu 450, 000 ambao hawana makazi maalum. Zaidi ya familia 18, 000 mjini Cebu zinahitaji msaada wa chakula, maji na dawa. Umoja wa Mataifa unasema kwamba, zaidi ya watu 10, 000 wamefariki dunia kutokana na maafa yaliyosababishwa na tufani iliyotokea hivi karibuni nchini Ufilippini.







All the contents on this site are copyrighted ©.