Majadiliano ya kidini yanalenga kuwasaidia watu kumfahamu Mungu
Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni kuanzia tarehe
14 hadi 16 Novemba 2013 yuko nchini Jamhuri ya wananchi wa Cheki kama sehemu ya mwendelezo
wa majadiliano ya kidini na waamini wasiomwamini Mungu. Akiwa nchini humo Kardinali
Ravasi amepangiwa ratiba ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa Serikali, wanadiplomasia,
wasomi na wanazuoni pamoja na wawakilishi kutoka katika dini na madhehebu mbali mbali
ya Kikristo n chini humo.
Kardinali Ravasi, Ijumaa tarehe 15 Novemba 2013
anatarajiwa kufanya majadiliano na wasomi mbali mbali kuhusiana na mambo ya imani
na malimwengu katika nyakati hizi. Hizi ni juhudi zilizoanzishwa na Baba Mtakatifu
mstaafu Benedikto wa kumi na sita, aliyetamani kuliona Kanisa la Kristo likiendeleza
majadiliano ya kidini na wale wasiomwamini bado Mungu, ingawa wana kiu na hamu ya
kusikia kweli za Kimungu katika hija ya maisha yao!