2013-11-14 14:29:56

Hakuna sababu msingi za kuogopa kuhusu vitisho vya Mafia dhidi ya Papa Francisko!


Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican amefafanua kwamba, Vatican haina sababu msingi za kuogopa vitisho vilivyosikika hivi karibuni kutoka kwa kikundi cha Mafia kwamba, mikakati ya kichungaji inayofanyiwa kazi na Baba Mtakatifu Francisko kwa sasa ya kutaka kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Kanisa, inaweza kugharimu maisha yake!

Baba Mtakatifu ataendelea na utume na maisha yake kadiri ya ushauri uliotolewa na Makardinali wakati wa mkutano elekezi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro na wala hakuna sababu ya kuogopa.

Baba Mtakatifu, Alhamisi 14 Novemba 2013 amefanya ziara ya kiserikali kwa kumtembelea Rais Giorgio Napolitano wa Italia, akisindikizwa na magari mawili tu ya vikosi vya ulinzi na usalama. Tukio hili limewashangaza wengi na kwa sasa ni sehemu ya gumzo ya vyombo vya habari na watu walioshuhudia akienda kumtembelea Rais Napolitano wa Italia.







All the contents on this site are copyrighted ©.