2013-11-14 11:56:36

Balozi mpya wa Vatican nchini Ujerumani awasili tayari kuanza utume wake!


Askofu mkuu Nikola Etrovic, Balozi mpya wa Vatican nchini Ujerumani aliyeteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 14 Novemba 2013 amewasili nchini Ujerumani tayari kuanza utume wake, kama Mwakilishi wa Vatican, baada ya kulitumikia Kanisa kama Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu Katoliki mjini Vatican.

Uwanja wa ndege wa Berlin- Tegel, Askofu mkuu Etrovic amepokelewa na viongozi mbali mbali wa Kanisa na Serikali kutoka Ujerumani, wakiongozwa na Kardinali Rainer Maria Woelk.







All the contents on this site are copyrighted ©.