2013-11-13 15:54:21

Papa aomba msaada kwa ajili ya wahanga wa maafa


Papa Francisko mara baada ya Mafundisho yake ya Jumatano , akiwa katika uwanja wa kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, alirudia kuiomba dunia, kutoa kwa ukarimu wote, msaada kwa watu walio sasa katika mahangaiko makubwa kutoka na maafa yaliyo nje ya uwezo wao, hasa huko Ufilipino.
Na pia aliionyesha kuguswa na janga la wanafunzi waliofariki huko Dameski kwa basi lao kulipuliwa na bomu wakati wakirejea toka shule na kusababisha maisha ya wanafunzi kadhaa na dreva wao kufariki na wengine wengi kujeruhiwa karibuni huko Dameski.
Kwa majonzi makubwa, Papa alikemea utendaji huo akisema kamwe na isitokee tena. Papa amemwomba Mwenyezi Mungu ayaepusha majanga haya yenye kuangamiza roho za binadamu, alizoziumba yeye mwenyewe.








All the contents on this site are copyrighted ©.