2013-11-13 15:27:33

Papa akutana na Askofu Mkuu Hilariòn Muotodosi wa Moscow


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne alikutana na Askofu Mkuu Hilarión , Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Nje kwa Kanisa la Kiotodosi la Urusi .

Na baadaye jioni, Askofu Mkuu Hilariòn alizindua kama ishara ya mazungumzo kati ya makanisa Katoliki na Kiorodisi, tamasha la Amani, lililofanyika kwa heshima ya Papa Francisko, lililofanikishwa na Kanisa Kiotodosi la Urusi, mkiandamana na nyimbo na muziki kutoka kwa vijana wa Kirusi, wakiongozwa na mwimbaji, Svetlana Kasyan, katika Ukumbi wa Mtaa wa Via della Conciliazione. Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni lilifadhili tamasha hili kwa lengo kukuza umoja wa Wakaristu. Na pia kwa ajili ya kufanikisha harambee ya kutoa msaada kwa kafara wa vita.
Makanisa haya mawili yalitengana miaka elfu moja iliyopta , lakini yakabaki katika hali ya kushirikishana mambo mengi, bila ya kukanusa tofauti zao. Hivyo inatumainiwa muziki, sanaa na nyimbo, vinaweza kuwa njia moja wapo ya kuimarisha umoja kati ya makanisa haya.
Roberti Moynihan wa Shirika la Urbi et Orobi la Marekani, akizungumza wakati wa tamasha hili, alilitaja kuwa ni sehemu ya safari ndefu ya mazungumzano kati ya makanisa haya mawili. Na kwamba, ingawa kunamatatizo ya kihstoria yenye kutia doa katika mahusiano, bado kuna mambo mengi ya kawaida msingi wanayoshirikishana , mfano kiimani na Sakramenti . Na daima wanajaribu kupata jawabu la kusogeleana karibu na karibu zaidi hata kitamaduni, na katika kutembea pamoja kwenye safari za kiroho,katika kumsifu Mungu pamoja na kushirikiana pia katika miradi fulanifulani pamoja na kuzungumzano ya pamoja katika neema ya amani na kukabiliana na changamoto nyingine kiliturujia zenye kuleta utengano kati ya makanisa haya mawili.
Kukutana kwa Papa Francisko na Askofu Mkuu Hilarión, kumefanyika wakati pia Askofu Mkuu wa Milan, Kardinali Angelo Scola , akiwa Moscow ,ambako naye amekutana na Mkuu wa Kanisa la Kiotodoksi la Urusi , Patriaki Kirill .

Juhudi hizi zinalenga kukuza umoja wa kiroho na maridhiano kati ya Waotodosi na Wakatoliki , na pia zinalenga kutazama kwa pamoja hali ya maisha katika Monasteri Wabenediktini nchini Ubelgiji , inajulikana kama Chevetogne Abbey. Monesteri Iliyo anzishwa mwaka 1920, ambayo anatunza mapokeo ya liturujia zote mbili Kilatini na Mashariki katika ibada zake za kila siku na pia ni mmliki wa jarida kongwe la kiekumeni duniani , linaloitwa ' Irenikon '.








All the contents on this site are copyrighted ©.