Maungamo ni ubatizo wa pili katika utakaso wa dhambi
Jumatano hii , Papa Francisko amewataka waumini wote kujenga tabia ya kuugama dhambi
kwa unyenyekevu na kuomba msamaha kwa Mungu , kila mara wanapotenda dhambi, ili kupata
neema za utulivu wa moyo na furaha. Wito huu ni sehemu ya ujumbe wa Papa kwa
waumini, ambao ameutoa kupitia Katekesi yake ya Jumatano, kwa mahujaji na wageni
, waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Alisema kama ilivyo
katika ubatizo ambamo dhambi ya asili na dhambi zingine hutakatifushwa, pia Sakramenti
ya Kitubio, hufungua mlango wa maisha mapya ya kiroho , wakati huruma ya Mungu inapoingia
ndani ya maisha yetu. Papa alieleza haya akiendelea kutafakari juu ya sala ya
Nasadiki, ambamo leo amegeukia Sakramenti ya Ubatizo, akisema, kila Jumapili wakati
wa kukiri imani yetu , tunasali: Nakiri katika ubatizo mmoja kwa msamaha wa dhambi.
Papa aliyatazama maneno hayo kwa kina na mara kutoa mwaliko kwa waliokuwa wakisikiliza,
kutafakari pamoja nae , neno hadi neno lililoandikwa katika aya hii. Alianza na neno
ninakiri, akisema, ni neno kuu linaloonesha umuhimu wa Ubatizo na kuthibitisha utambulisho
cha mbatizwa kuwa mtoto wa Mungu. Katika Sakramenti , imani yetu pia inahusishwa na
maondoleo la dhambi. Tunapo ungama dhambi zetu , pia tunafanywa upya kiroho na kuimarisha
utambulisho wa ubatizo wetu. Na hivyo basi , ubatizo , inakuwa ni mahali pa kuuanza
mwendo wa safari ndefu ya maisha yote ya uongofu endelevu, yanayolishwa na Sakramenti
ya Kitubio . Na maneno Ubatizo Mmoja – ambamo neno ubatizo linamaanisha kuzamisha,
kwa njia ya Sakramenti hii, muumini huizamisha roho yake katika kifo cha Yesu Kristo,
na kufufuka naye kama kiumbe kipya. Akiwa amefanywa upya na maji na Roho Mtakatifu
, humlikiwa na mwanga wa neema ambayo hufukuza uvuli wa dhambi. Papa Francisko
aliendelea kueleza kwamba, kwa maneno kwa msahama wa dhambi,maneno haya yanaonyesha
kwamba, Ubatizo huondoa dhambi ya asili na dhambi ya nyingine binafsi. Na hivyo ,
kwa ubatizo, mlango kwa maisha mapya hufunguliwa na huruma ya Mungu huingia katika
maisha yetu. Lakini , Papa alionya kwamba udhaifu wa binadamu hubaki palepale. Ndiyo
maana kanisa linatufundisha kuungama dhambi zetu kwa unyenyekevu mara kwa mara ,
kwa sababu tu katika msamaha,tupewana kupokea neema ya kuifanya mioyo yetu yenye kuhangaika
daima, kupata amani na furaha.