Maaskofu wa Ufilipino watoa wito wa Novena kwa wahanga wa Kibunga.
Maaskofu Katoliki wa Ufilipino, wametoa wito wa Novena, sala na fadhila, kwa waathirika
na familia zilizopigwa vikali na maafa ya kimbunga kilichopita hivi karibuni na kuua
mamia ya watu na kuharibu mali nyingi, zikiwemo nyumba.
Mosinyori Pedro Quitorio
, Mkurugenzi wa vyombo vya habari katika Baraza la Maaskofu Katoliki ya Philippines
, alisema fedha zitakazo tolewa wakati wa kipindi cha Novena , iliyoanza Jumanne
12 na itaendelea hadi Novemba 19, zitaelekezwa katika Majimbo yaliyo athirika zaidi
na kibunga kupitia tawi la Caritas Ufilipino. Na alitaja majimbo yaliyopigwa zaidi
kuwa ni Jimbo la Borongan na Jimbo Kuu la Palo .
Katika jimbo la Borongan
, ambako kibunga kilianzia , kimeharibu pia kanisa kongwe lililo tajwa na UNESCO,
kuwa urithi wa duniani, ambalo liliwaka moto na kuharibiwa karibia kwa 85-95 pamoja
na nyumba zilizokuwa katika parokia hiyo pia zimeharibiwa, ingawa kwa jinsi ilivyofanyika,
kunaleta utata wa kujiuliza maswali mengi juu ya hilo. Katika mkoa wa Palo , ambako
kuna mji wa Tacloban , watu wengi wamefariki duniani. Askofu Quitorio anasema , ingawa
miundombinu na kanisa mengi yameharibiwa , ikiwa pamoja na Makao Makuu ya Palo na
kaburi muhimu ya Mtakatifu Nino. Kipaumbele kwa wakati huu ni ksaudia watu kuishi
na sio majengo.
Na akizungumzia haja ya kupeleka viongozi zaidi wa kiroho
katika eneo hilo anasema, ni vyema kufanya hivyo. Lakini kwa wakati huu kinachohitajika
zaidi ni kukusanya fedha kwa ajili ya upatikanaji wa msaada wa kwa ajili ya chakula
, maji na dawa.
Licha ya hivyo , kw awakati huu katika badhi ya miji iliyokubwa
hakuna tena utaratibu wa kiserikali, watu wanapora vitu , wanaingia k tiak mafuka
wakitafuta chakula chao. Hakuna sheria na utaratibu hivi sasa. Hii ni wasiwasi wetu
wa kwanza. Serikali haijaweza kusitisha uasi huu . Kanisa linatumaini , serikali itawweza
kurejesha amani na utulivu haraka iwezekanavyo, na hasa katika tararibu za msaada
unaotolewa kuwafikia wahitaji wote bila usumbufu mkubwa.