2013-11-12 15:22:38

Papa ahimiza, tujikabidhi katika Mkono wa Mungu aliyetuumba


Sote ni lazima tutaipita njia ya kifo. Na ni muhimu kutambua kwamba, katika maisha haya kuna njia mbili, moja ni njia inayongoonzwa na shetani na njia nyingine ni ile inayo elekea kwa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko ameeleza katika homilia yake, wakati wa Ibada ya misa mapema Asubuhi, Jumanne hii katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta la hapa Vatican.
Papa amesema, Biblia inaelezea kinaga ubaga, juu ya uumbaji wa Mungu , ambao, kwa mikono yake alituumba sisi sote kutoka matope ya nchi, kwa sura na mfano wake. Na hivyo kwa mikono yake Mungu alituumba kwa ustadi mkuu. Lakini sisi binadamu bila kujali tunalisahau hilo na kuitelekeza mikono ya Mungu iliyotuumba, tukiiacha njia yake na kutembea katika nji aya mwovu shetani.
Lakini Mungu aliye Baba yetu , kama baba na mtoto wake , anaendelea kutufundisha kutembea katika njia ya maisha inayoongoza katika wokovu. Ni mikono ya Mungu inayo tubembeleza na kuturiwaza nyakati za mahangaiko na mateso na huzuni kuu za maisha. Kwa mwenye kuishi na Mungu, huuona upendo huu na Mungu uliojaa neema na faraja kuu. Huwa na baba anayembeleza kwa upendo mkuu.
Papa aliendelea kuasa kwamba kwa bahati mbaya , pamoja na kutubembeleza na kutuhakikishi ayu pamoja nasi ktika nyakati zote , bado tunamwasi na kumsea kwa mara nyingi , lakini Yeye hutuvumilia na hachoki kutusamehe.
Papa alitoa ushuhuda wake kwamba, kwake yeye furaha yake na matumaini yake kwamba, daima huguswa na utendaji wa Yesu ambaye pamoja na kukataliwa na kupambana na mateso makubwa, aliendelea na mpango wake wa kutuongoza kwa Muungu Baba hadi kifo cha msalabani, kuzikwa na kufufuka kwa ajili yetu. Na hivyo kwa gharama ya mikono yake iliyo jeruhiwa kwa ajili ya kutupenda sisi, tunapata mastahili yakuitwa pia watoto wa Mungu. Hii ni faraja kuu.

Papa Francisko aliendelea kuitafakari Mikono ya Yesu, wakati ikigusa wagonjwa na kuwaponya, ni mikono hiyohiyo ambayo hata sisi leo hii tukiamini na kulishi neno lake inatuponya na kutuongoza kwa Mungu. Papa anaona kwa upendo alio nao Mungu kwa binadamu, ni vigumu kufikiri kwamba Mungu anaweza kumpiga kofi mtu. Mungu ambaye ni upendo daima badala yake, hutubembeleza na kutufariji wakati wa uchungu na huzuni. Nafsi za wenye haki ziko katika mikono yake Mungu. Mikono ya Mungu aliye tuumba kwa ustadi, ni hiyohiyo inayotupa wokovu wa milele, iwapo tutamwamini. . Ni Yeye aliyejuruhiwa mikono anayetuongoza katika njia hii ya maisha yanayoelekea katika wokovu.
Papa alikamilisha homilia kw kutoa wito kwa kila binadamu, kuona vyema kujikabidhi katika mikono ya Mungu , kama mtoto mdogo anavyo jiaminisha katika mikono ya baba yake. Mkono wa Mungu ni Mkono wa uhakika.








All the contents on this site are copyrighted ©.