2013-11-12 07:22:14

Papa achangia kiasi cha dolla za Kimarekani 150, 000 kwa wahanga wa maafa nchini Ufilippini


Baba Mtakatifu Francisko kwa kuguswa na mahangaiko pamoja na mateso ya wananchi wa Ufilippini waliokumbwa na maafa ya kimbunga cha Hayain hasa katika visiwa vya Leyte na Samar na kusababisha zaidi ya watu elfu kumi kupoteza maisha, ametoa kiasi cha dolla za Kimarekani, 150, 000, kama awamu ya kwanza ya mchango wake kwa waathirika wa maafa haya.

Mchango huu umetolewa na Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki Cor Unum. Fedha hizi zitatolewa kwa Kanisa mahalia, ili kusaidia watu walioathirika kwa mafuriko. Hiki ni kielelezo cha imani tendaji, kama njia ya kuonesha uwepo wake wa karibu kwa watu wananchi waliokumbwa na maafa.







All the contents on this site are copyrighted ©.