2013-11-12 07:12:27

Onesheni moyo wa sala na ukarimu kwa wananchi wa Ufilippini na Vietnam waliofikwa na maafa!


Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kufuatilia kwa karibu mateso na mahangaiko ya wananchi wa Ufilippini pamoja na Vietnam waliokumbwa na kimbunga cha Haiyan, kinachoendelea kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wengi Barani Asia.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika kwa namna ya pekee kuwakumbuka katika sala na matendo ya huruma wananchi wa Ufilippini na Vietnam, ambao kwa sasa wanakabiliana na hali ngumu ya maisha baada ya maafa yaliyosababishwa na kimbunga cha Haiyan.







All the contents on this site are copyrighted ©.